1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinzi mazingira waandamana

9 Desemba 2007

---

BALI:

Watetezi wa usafi wa mazingira ulimwenguni, waliandamana jana katika miji 50 mbali mbali duniani katika siku ya kuchukua hatua kivitendo kulinda mazingira.

Mjini Berlin, Ujerumani, kiasi cha waandamanaji 5000 walisimama mbele ya lango mashuhuri la „Brandenburg Gate“ wakidai kupunguzwa kwa moshi unaochafua hewa.

Jioni ya jana, katika majumba na maafisi sehemu kubwa ya Ujerumani, taa zilizimwa kwa muda wa dakika 5 kubainisha jinsi umeme unavyopotezwa bure.

Taa za mwanga mkubwa katika lango la BrandenburgGate na katika qasri la Neueschwanstein huko Bavaria pia zillizimwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW