1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinzi wa pwani Libya waokoa wahamiaji karibu na Tunisia

17 Julai 2023

Wizara ya mambo ya ndani ya Libya imesema leo kuwa walinzi wa mipakani wamewaokoa mamia ya wahamiaji wa Kiafrika wanaosema wamefukuzwa na mamlaka za Tunisia.

Migranten auf den Kanaren
Picha: Manuel Navarro/dpa/picture alliance

Wahamiaji hao walipatikana jangwani na kupelekwa katika kijiji cha al-Assah kilichoko katika eneo hilo la mpaka. 

Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa kundi la maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, na mamlaka za Libya waliwapa wahamiaji haochakula, nguo na makaazi ya muda pamoja na huduma za kwanza za matibabu kwa waliojeruhiwa.

Soma pia:Tunisia: Wahamiaji wasio na vibali walitumiwa dola bilioni 1 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023

Katika video iliyochapishwa na wizara hiyo, wanaume wawili kutoka Nigeria wamesema walipigwa na wanajeshi wa Tunisia na kupelekwa pamoja na wahamiaji wengine katika eneo la jangwa na kuamrishwa kuvuuka mpaka kuingia Libya.

Mwanamme mwingine amesema wanajeshi hao wa Tunisia walichukuwa paspoti zao na kuzichoma kabla ya kuwasafirisha watu 35 katika gari moja kuelekea katika eneo hilo la mpaka na Libya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW