1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUgiriki

Waliofariki katika ajali ya treni Ugiriki wapindukia 42

2 Machi 2023

Idadi ya vifo kufuatia ajali ya mbaya ya treni nchini Ugiriki imeongezeka na kufikia watu 42, huku matumaini ya kuwapata manusura wakiwa hai yakizidi kufifia.

Kyriakos Mitsotakis | griechischer Ministerpräsident
Picha: Giorgos Kontarinis/ANE Edition/Eurokinissi/IMAGO

Waziri Mkuu wa ugiriki Kyriakos Mitsotakis ameitaja kuwa ajali mbaya ya treni isiyo na mfano na kuahidi kuwa mkasa huo utachunguzwa kikamilifu.

Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Treni iliyokuwa imebeba abiria 350 ilikuwa inatoka Mji Mkuu Athens na kuelekea mji wa kaskazini wa Thessaloniki iligongana na nyingine ya mizigo usiku wa Jumanne karibu na mji wa Larissa.

Waziri wa uchukuzi wa Ugiriki aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu saa chache baada ya ajali hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW