1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Waliokufa katika mzozo wa mgodi Afrika Kusini wafika 87

16 Januari 2025

Idadi ya waliofariki katika mzozo wa miezi kadhaa kati ya polisi na wachimba migodi Afrika Kusini imeongezeka na kufikia 87.

Afrika Kusini | Kufungwa kwa mgodi uliotelekezwa wa Stilfontein
Wachunguzi wakibeba miili kwenye mifuko wakati wa operesheni ya kuwaokoa wachimbaji madini mgodini eneo la Stilfontein, Afrika KusiniPicha: Themba Hadebe/AP Photo/picture alliance

Hayo yamesemwa siku ya Alhamisi na polisi wakati wakihitimisha operesheni ya uokoaji ambayo imewaondoa mgodini zaidi ya manusura 240.

Msemaji wa polisi ya kitaifa Athlenda Mathe amesema miili 78 iliondolewa kwenye mgodi huo katika operesheni rasmi iliyoanza Jumatatu, na nyingine ilikuwa imepatikana hapo awali. Bibi Mathe hakutoa maelezo ya jinsi miili hiyo ilivyopatikana.

Mashirika ya kijamii yamesema yalianzisha pia juhudi zao za uokoaji wakati maafisa waliposema mwaka jana kuwa wasingewasaidia wachimbaji hao kwa sababu ni wahalifu. Wachimba migodi hao wanasemekana kufariki kutokana na njaa na upungufu wa maji mwilini.

Maafisa sasa wanaamini kuwa karibu wachimbaji 2,000 walikuwa mgodini humo kinyume cha sheria tangu Agosti mwaka jana. Wengi wao walitoka kwa hiari yao katika miezi michache iliyopita, na manusura wake wamekamatwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW