1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waliokufa kwa tetemeko Japan wafikia 62

3 Januari 2024

Waokoaji wa Japan wapo katika juhudi za kuwatafuta manusura wa tetemeko la ardhi la maadhimisho ya Siku ya Mwaka Mpya lililoua takriban watu 50 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Japan Erdbeben Januar 2024
Nyumba zilizobomolewa na tetemeko la ardhi la JapanPicha: Buddhika Weerasinghe/Getty Images

Tetemeko kubwa la ardhi  lililofikia kipimo cha 7.6 katika jimbo la Ishikawa lilisababisha mawimbi ya tsunami yenye urefu wa zaidi ya mita moja, na kusababisha moto mkubwa na kusambaratisha barabara.Katika eneo la Noto, uharibifu ulijumuisha majengo yaliyoharibiwa na moto, nyumba kusambaratishwa, boti za uvuvi kuzama au kusombwa ufukweni, na barabara kuu zilizovunjika na maporomoko ya ardhi. Shirika la habari laJapanKyodo limeripoti watu walokufa wamefikia 57. Mwaka 2011, nchi hiyo kwa upande wa kaskazini/mashariki ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la ukubwa wa 9.0 katika kipimo cha Richter,  ambalo lilisababisha tsunami iliyosababisha vifo vya takriban watu 18,500.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW