1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waliokufa mashambulizi ya msikitini Pakistan wafikia 100

1 Februari 2023

Shambulizi la kujitoa muhanga lililotokea ndani ya msikiti ulioko katika makao makuu ya polisi nchini Pakistan mapema wiki hii lilikuwa la kulipiza kisasi.

Pakistan Peshawar Explosion der Polizeilinie
Picha: Faridullah Khan/DW

Muhammad Ijaz Khan, afisa mkuu wa polisi katika mji huo, amesema hayo mnamo wakati idadi ya vifo imefikia 100 baada ya juhudi za uokozi kumalizika.

Ijaz Khan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kama polisi wako mstari wa mbele dhidi ya wanamgambo, na ndiyo sababu walilengwa.

"Lengo la shambulizi lilikuwa ni kuwavunja moyo." Alisema.

Kati ya maafisa wa polisi 300 hadi 400 walikuwa wakiswali kwenye msikiti huo siku ya Jumatatu wakati shambulizi lilipotokea.

Mashambulizi hudaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo la Taliban la Pakistan na vile vile tawi la kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini humo, lakini shambulizi linalosababisha vifo vingi kama hilo hutokea kwa nadra.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW