1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

IBUKA: Afisa wa zamani amekufa kabla ya haki kutendeka

10 Desemba 2023

Kundi la watu walionusurika na mauaji ya kimbari ya Rwanda IBUKA wamelaani kifo cha afisa wa zamani aliyehukumiwa kwa mauaji ya kimbari kabla ya haki kamili kutendeka.

Rwanda, mauaji ya kimbari
Sehemu ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda Picha: Sayyid Abdul Azim/AP/picture alliance

Mwenyekiti wa chama cha walionusurika na mauaji hayo Philibert Gakwenzire amesema, licha ya uhalifu wa kutisha Bucyibaruta aliishi maisha mazuri bila haki kutendeka.

Soma zaidi: Daktari afikishwa mahakamani Ufaransa kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda

Afisa huyo wa zamani  Laurent Bucyibaruta aliyefariki dunia Jumatano akiwa na miaka 79, alikuwa mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu zaidi wa Rwanda kujibu mashtaka huko Ufaransa katika kesi ya mauaji ya kimbariyaliyowauwa karibu Watutsi 800.000.

Alikutwa na hatia ya kuhusika na mauaji hayo na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika matukio manne ya mauaji ya halaiki Kusini mwa mkoa wa Gikongoro Julai 2022 na alihukumiwa kwenda miaka 20 jela. Hata hivyo mahakama ilimuachilia huru baada ya kukata rufaa huku akisubiri kusikilizwa kwa kesi mpya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW