1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliotekwa nyara Nigeria siku ya pasaka waokolewa

6 Aprili 2026

Jeshi nchini Nigeria limesema limewaokoa waumini 31 wa dini ya kikristo waliotekwa katika sherehe za Pasaka katika eneo lililopo kaskazini magharibi mwa jimbo la Kaduna.

Nigeria Kaduna 2024 | Nigeria
Gari la jeshi katika jimbo la Kaduna, Nigeria Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Jeshi nchini Nigeria limesema limewaokoa waumini 31 wa dini ya kikristo waliotekwa katika sherehe za Pasaka katika eneo lililopo kaskazini magharibi mwa jimbo la Kaduna. 

Taarifa hiyo ya jeshi imeongeza kwamba vikosi vyake viliwakabili washambuliaji hao katika mapigano makali na yaliyowafanya magaidi kukimbia na kuwaacha mateka hao. Utekaji huo ulitokea katika kijiji cha Ariko kilichopo karibu kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu, Abuja.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakristo wa Nigeria wa jimbo la Kaduna, Caleb Bawa Ma'aji, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu saba  waliuawa katika mkasa huo ingawa taarifa yake inakinzana na ile jeshi ambayo imesema ni watu watano.

Kaduna ni miongoni mwa majimbo ya kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakitishiwa na magenge ya wahalifu ambayo hufanya uvamizi na utekaji nyara kwenye jamii na baadaye kudai fidia ili kuwaachilia mateka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW