Waliouawa maandamano DRC wazikwa
19 Septemba 2023Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kongo, Peter Kazadi, alisema siku ya tarehe 30 Agosti wanajeshi wa Kongo waliwafyatulia risasi waandamanaji mjini Goma na kuwauwa 57 kati yao.
Siku ya Jumatatu (Septemba 18), Kazadi alikwenda Goma kukutana na familia za wahanga na kusimamia shughuli ya mazishi.
Soma: Wataalam wa UN waeleza jinsi Rwanda imehusika na mzozo DRC
DR Congo: Mzozo uliopuuzwa
Waziri huyo alisema miili, ambayo ilikuwa ikioza kwenye hospitali ya kijeshi ya Goma kwa siku 20, ilikuwa ikisababisha hatari za kiafya.
Ndugu za wahanga hao walizuiwa kuitembelea hospitali hiyo tangu mauaji yalipofanyika hadi Septemba 12.
Kwa mujibu wa Kazadi, serikali imetoa majeneza, imelipia gharama za mazishi na kutoa mkono wa pole kwa ajili ya kuzifariji familia za wahanga.