1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamalawi wanapiga kura kumchagua rais

Sekione Kitojo
23 Juni 2020

Wamalawi wanamchagua rais

Malawi Wahlen
Picha: picture-alliance/AP Photo/T. Chikondi

Wananchi wa Malawi wanapiga  kura leo katika uchaguzi wa rais unaorudiwa  baada  ya mahakama kubatilisha matokeo  ya  uchaguzi  uliofanyika mwaka  mmoja  uliopita. Mahakama ya  katiba  hapo Februari 3 iliamuru  kuwa uchaguzi  huo urudiwe, ikiamua  kuwa  matokeo  ya uchaguzi  wa  mwanzo yamebatilishwa kwasababu  ya ushahidi mkubwa  wa  mapungufu  pamoja  na  kughushi kura  katika  uchaguzi  uliofanyika  Mei 2019.

Mahakama  ilibatilisha  ushindi  wa  rais  aliyeko madarakani Peter Mutharika ikielezea  ushahidi mkubwa wa udanganyifu katika  upigaji  kura, ikiwa  ni  pamoja  na maelfu  ya  kura  ambazo zilionekana  kubadilishwa  kwa kutumia wino wa  kufanyia  masahihisho. Hukumu  hiyo ilikubaliwa na  mahakama kuu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW