Wamarekani waanza kurejea katika maisha yao.
31 Oktoba 2012Kimbunga Sandy kimeathiri usafiri wa umma pamoja na mfumo wa nishati umeme kwa kiasi kikubwa katika maeneo kadhaa ya jiji la New York na itachukua siku kadhaa pia kurejeshwa kwake katika hali ya kawaida. Ikiwa ni siku sita kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani, yaani Novemba 6, Rais Barack Obama atatembelea eneo ambalo limevurugwa kabisa na kimbunga hicho la ufukwe wa New Jersey.
Katika ziara yake hiyo ataongozwa na Gavana wa eneo hilo ambae anatoka chama cha Republican Chris Christie ambae anamuunga mkono mpinzani wake Mitt Romney ambae hata hivyo amemsifu Obama na Juhudi za serikali katika kukabiliana na kimbunga hicho.
Mazingira magumu kwa Romney
Kadhia hii imemuweka katika mazingira magumu ya kisiasa Romney ambae mwaka uliyopita alinukuliwa akisema shirika la serikali la kukabiliana na majanga ya dharura lifungwe na majukumu yake yaachwe kwa majimbo husika. Na sasa imebakia wiki kabla ya uchaguzi ukiwa unakwenda sawia na janga hilo kubwa la kimbunga. Kampeni ya Romney inawahikishia wapiga kura kwamba utawala wake utahakikisha waathiriwa wa majanga hawateseki.
Viongozi katika ngazi zote wana kazi kubwa sana kurejesha katika hali ya kawaida maeneo yenye wakazi wengi yalikuwa katika pwani ya Mashariki nchini Marekani.
Kimbunga Sandy kinakadiriwa kugharimu maisha ya watu wa 40 nchini humo,na kupiga kutoka kutoka upande wa majini na kutpa theluji katika milima ya Milima ya Apalachian, zaidi ya makazi ya watu milioni 8.2 sambamba na maeneo ya biashara yalibaki pasipo umeme katika majimbo kadhaa.
Hali mbaya New York
Njia za reli na barabara ambazo zinatumiwa na idadi kubwa sana ya watu jijini New York zilijaa maji. Nusu ya eneo la Manhattan limeendelea kutokuwa na umeme baada ya kutokea mripuko katika kituo kidogo cha umeme kinachohudumia eneo hilo Con Edison.
Kimbunga hicho kilisukuma maji katika jiji la New York kwa urefu wa futi 14 na kwamba kutokana na hilo jiji hilo, serikali inasema wakazi wake wataendelea kutabika pasipo kutumia njia za chini zenye umuhimu mkubwa kwa siku kadhaa.
Usafiri wa mabasi una mipaka yake kwa hivyo watu wengi wanatembea umbali mrefu kwa miguu au kutumia taxi katika mitaa ya jiji hilo.
Mwandishi: Sudi Mnette/AFP/APE
Mhariri:Yusuf Saumu