Wamarekani wajiandaa kumchagua rais mpya Novemba 5
4 Novemba 2024Matangazo
Makamu wa Rais wa sasa Kamala Harris kutoka chama cha Democratic anachuana na rais wa zamani Donald Trump wa Republican kuwania funguo za ikulu ya White House baada ya karibu mwaka mmoja wa kampeni.
Zaidi ya Wamarekani milioni 77 tayari wamekwishapiga kura mapema na wagombea hao wawili wanatumai kuwahimiza mamilioni wengine kujitokeza kwa wingi kesho Novemba 5.
Soma pia:Wafahamu wagombea urais Marekani na sera zao
Wagombea wote wawili wanataitumia siku ya mwisho ya kampeni kwenye jimbo la Pennsylvania ambalo ni miongoni mwa yale machache yasiyotabirika yatakayoamua mshindi wa uchaguzi wa kesho.
Uchunguzi wa maoni ya umma unaonesha ushindani bado ni mkali baina ya wagombea hao wawili na ni vigumu kubashiri mwanasiasa anayeibuka mshindi.