1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamarekani wanapiga kura

8 Novemba 2022

Wapiga kura nchini Marekani leo wanashuka katika vituo vya kupiga kura katika uchaguzi wa bunge wa katikati ya muhula wa taifa hilo ambao utakuwa na athari kubwa katika miaka miwili ya mwisho ya Rais Joe Biden.

US Zwischenwahlen 2022
Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Wapiga kura nchini Marekani leo wanashuka katika vituo vya kupiga kura katika uchaguzi wa bunge wa katikati ya muhula wa taifa hilo ambao utakuwa na athari kubwa katika miaka miwili ya mwisho ya Rais Joe Biden. 

Wapiga kura wanaostahiki wataamua walio wengi katika Bunge la Marekani -mabaraza mawili ya sheria ya nchi yaani Baraza la Wawakilishi na Seneti, sawa na kuwachagua wabunge na maseneta pamoja na kuamua juu ya ugavana na ofisi nyingine muhimu.

Wapiga kura wanaweza kutoa adhabu kwa chama cha Democrat, ambacho kwa wakati huu kinadhibiti Ikulu na Bunge la Marekani, kutokana na kile kinachoonekana hali ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei na kuyumba kwa uchumi. Kwa kawaida chama kilicho madarakani katika kipindi kama hichi cha ucahguzi kinapoteza nguvu zake.

Matarajio ya Trump kupanda nguvu zaidi bungeni.

Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Gaelen Morse/REUTERS

Na endapo katika uchaguzi huu chama cha Democrat kitapoteza wingi wa kura bungeni, wapinzani wao wa Republican watakuwa na uwezo wa kuzuia sera nyingi za Biden hadiuchaguzi wa rais ujao wa Novemba 2024. Kwa mujibu wa  kura za maoni, kuna uwezekano wa Baraza la Wawakilishi kwenda kwa Republican. Lakini katika Seneti, kunatarajiwa mjongeleano wa karibu.

Katika siku ya mwisho ya kampeni rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema juma lijalo atatoa tangazo zito katika kipindi hichi ambacho amedokeza kuwania mara ya tatu urais wa Marekani. Huu ni mwaka ambao tutarudisha Bunge. Tutachukua tena Seneti na tutairudisha Marekani. Na ukiwadia mwaka 2024, la muhimu zaidi, tutairudisha Ikulu kwa namna fahari kubwa.."

Soma zaidi:Biden, Trump wafanya kampeni za mwisho kuelekea uchaguzi wa katikati ya muhula

Kiongozi huyo wa zamani wa Marekani ameonekana akiweka wazi zaidi mipango yake ya kuwania muhula mwingine, akisema kuna uwezekano mkubwa kukamilisha nia yake.  Kimsingi uchaguzi huu wa leo unahusisha viti  jumla 435 vya Baraza la Wawakilishi lakini lile la Baraza la seneti, viti  35 kati ya idadi jumla ya viti 100 vya baraza hilo.

Kwa hivyo taswira kamili ya uchaguzi huu wa katikati ya muhula wa mabunge ya Marekani itaonesha wazi endapo Trump, atapata nafasi ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2024.

Vyanzo: AP/DAP/DW