1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMauritania

Wamauritania wapiga kura kumchagua rais mpya

29 Juni 2024

Raia wa Mauritania wanapiga kura Jumamosi katika uchaguzi ambao rais aliyeko madarakani Mohamed Ould Ghazouani anachuana na wapinzani sita katika taifa hilo la jangwa la Afrika Magharibi.

Uchaguzi Mauritania
Watu milioni 2 wamesijiliwa kupiga kura katika nchi ya Mauritania yenye wakaazi milioni 5Picha: Med Lemine Rajel/AFP

Ghazouani, mwenye umri wa miaka 67, mwanajeshi wa zamani wa ngazi ya juu, ameahidi kuharakisha uwekezaji ili kuchochoea uongezeko la bei na mahitaji ya bidhaa muhimu katika nchi hiyo yenye watu milioni tano, wengi wao wakiishi katika umaskini licha ya utajiri wake wa mafuta ya kisukuku na madini.

Soma pia: Rais wa Mauritania anatoa wito kwa mataifa ya Afrika Magharibi kushirikiana dhidi ya itikadi kali

Ghazouani ambaye alichaguliwa kwa muhula wa kwanza mwaka wa 2019, anatarajiwa na wengi kushinda uchaguzi wa Jumamosi kutokana na umaarufu wa chama tawala. Wapinzani wake sita ni pamoja na mwanaharakati anayepinga utumwa Biram Dah Abeid, aliyemaliza wa pili mwaka wa 2019 na asilimia 18 ya kura, mwanasheria Id Mohameden M'Bareck, mchumi Mohamed Lemine El Mourtaji El Wafi na Hamadi Sidi El Mokhtar wa chama cha Tewassol. Watu milioni 2 wamesijiliwa kupiga kura. Masuala muhimu kwao yanajumuisha vita dhidi ya ufisadi na kutengenezwa nafasi za ajira kwa vijana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW