1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

Wamexico wapiga kura katika katika uchaguzi wa kihistoria

2 Juni 2024

Claudia Sheinbaum, mgombea wa chama tawala, Movement for National Regeneration (Morena), yuko katika nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi na Xochitl Galvez anawakilisha vuguvugu la vyama vya mrengo wa kulia.

Wagombea wa Urais Mexico wakishiriki kwenye mdahalo
Wagombea wa Urais Mexico wakishiriki kwenye mdahaloPicha: Quetzalli Nicte-Ha/REUTERS

Wagombea wakuu wawili wote ni wanawake. Claudia Sheinbaum, mgombea wa chama tawala, Movement for National Regeneration (Morena), yuko katika nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi na kuchukua nafasi ya Rais anayemaliza muda wake Andres Manuel Lopez Obrador.

Kwa upande wake mgombea wa upinzani, mfanyabiashara na seneta wa zamani, Xochitl Galvez anawakilisha vuguvugu la vyama vya mrengo wa kulia. Karibu Wamexico milioni 100 watachagua hii leo rais wao mpya, wabunge, maseneta na viongozi wa mikoa na manispaa.

Hata hivyo kampeni ya uchaguzi ilighubikwa na visa vya ghasia na machafuko. Mgombea mmoja wa umeya aliuawa katikati mwa Mexico siku ya Ijumaa, siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na mauaji ya angalau wafuasi 34 wa kisiasa.

Viongozi wanasema mashambulizi haya yanafanywa na vikundi vya uhalifu vinavyopigania ushawishi katika baadhi ya mikoa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW