1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamisri 5 na Wazambia 6 wafikishwa mahakamani Lusaka

29 Agosti 2023

Raia watano wa Misri na Wazambia sita wamefikishwa mahakamani baada ya ndege kutua mjini Lusaka ikiwa na kilo 130 za dhahabu.

Washukiwa wanahusishwa na ndege iliyotua Lusaka ikiwa na kilo 130 za dhahabu na inaripotiwa ndege hiyo ilipitia Cairo.
Washukiwa wanahusishwa na ndege iliyotua Lusaka ikiwa na kilo 130 za dhahabu na inaripotiwa ndege hiyo ilipitia Cairo.Picha: Amir Makar/AFP/Getty Images

Maafisa wa Zambia walikamata pia risasi 126 na karibu dola milioni 5.7 wakati ndege hiyo ilipotua Lusaka wiki mbili zilizopita.

Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya imesema washukiwa 11, ikiwa ni pamoja na afisa mwandamizi wa polisi wa Zambia, wamekamatwa na kushtakiwa kwa ujasusi.

Kulingana na mamlaka hiyo, ni kwamba ndege hiyo iliyokodishwa ilikuwa ikisafirisha bidhaa hatari.

Mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Misri ambaye alikamatwa mjini Cairo kufuatia ripoti za kuwatuhumu maafisa kuhusika na magendo ya fedha, silaha na dhahabu, aliachiliwa huru baadaye.

Hata hivyo, vyombo vya habari vya Misri vilidai kuwa ndege hiyo inamilikiwa na watu binafsi na kwamba Cairo ilipitia tu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW