Wana anga waliosafiri karibu na mwezi warejea duniani
11 Aprili 2026
Shirika la anga la Marekani, NASA, limesema wanaanga wanne wa mradi wa Artemis 2 waliokuwa kwenye chombo cha Orion, Christina Koch, Victor Glover na Reid Wiseman raia wa Marekani, na mwenzao Jeremy Hansen kutoka Canada walitua jana jioni katika eneo la Pasifiki karibu na San Diego kama ilivyopangwa.
Baada ya kutua kwao, timu ya maafisa wa NASA na wa idara ya ulinzi ya Marekani waliwasaidia kutoka kwenye chombo hicho cha Orion na kuwasafirisha kwa helikopta hadi katika meli maalum.
Mkuu wa NASA Jared Isaacman, amewapongeza wana anga hao na kutaja tukio hilo kuwa la kihistoria.
NASA pia imesema watafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kurejehswa Houston.
Wakati huo huo, katika chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Rais wa Marekani Donald Trump ametaja safari hiyo ya mwezini kuwa ya kipekee na kutua kwako kuwa thabiti.