1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Wanadiplomasia wa China na Japan wakutana kwa mazungumzo

25 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amekutana na yule wa Japan Yoko Kamikawa ili kujadili changamoto za kikanda na kimataifa.

Südkorea | Die japanische Außenministerin Yoko Kamikawa (l.) führt ein Gespräch mit ihrem chinesischen Amtskollegen Wang Yi
Mawaziri wa mambo ya nje wa Japan Yoko Kamikawa (Kushoto) na wa China Wang YiPicha: Kyodo/picture alliance

Wanadiplomasia wakuu kutoka Japan na China wamekutana kwa mazungumzo leo Jumamosi huku wakijaribu kusuluhisha mizozo kati ya mataifa hayo mawili ikiwa ni pamoja na marufuku ya China kuhusu uuzaji wa bidhaa za baharini za Japan.

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amekutana na yule wa Japan Yoko Kamikawa katika mji wa mwambao wa Korea Kusini wa Busan ambako wanadiplomasia wakuu wa China, Japan na Korea Kusini wanatarajiwa kukutana kesho ili kujadili changamoto za kikanda na kimataifa.

China ilichukua hatua hiyo baada ya kinu cha nyuklia cha Fukushima kuanza mnamo Agosti 24, kumwaga baharini taka za nyuklia zisizokuwa na mionzi. Japan imekuwa ikijitetea kuwa maji kutoka kinu hicho ni salama zaidi kuliko viwango vilivyowekwa kimataifa, madai yaliyopingwa na Beijing.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW