1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi 120 hawajulikani walipo baada ya shambulio Nigeria

7 Julai 2021

Karibu wanafunzi 125 bado hawajulikani waliko, lakini wengine 28 wameshapatikana kuunganishwa tena na familia zao baada ya shambulio la watu wenye silaha katika bweni la shule katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria.

Nigeria Kaduna | Entführung Schüler | Versammlung der Eltern
Picha: KEHINDE GBENGA/AFP

Mkuu wa Kanisa la Ubatizo jimboni Kaduna nchini Nigeria amesema karibu wanafunzi 125 bado hawajulikani walipo hadi Jumatano, lakini wengine 28 wameunganishwa tena na familia zao baada ya shambulio la watu waliojihami kwa silaha dhidi ya shule ya bweni jimboni humo.

Washambuliaji hao waliivamia shule ya sekondari ya Bethel Baptist siku ya Jumatatu, katika tukio la kumi la utekaji wa wanafunzi wa shule tangu Desemba katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Nigeria.

Wazazi waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kawaida wanafunzi 180 wanahudhuria shuleni hapo, na kwamba walikuwa kwenye mchakato wa kufanya mitihani.

nchini Nigeria, zimehusisha matukio hayo ya utekaji nyara na kile wanachokiita majambazi wanaotafuta malipo ya kikomboleo. Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, linakadiria kwamba takribani shule 1,120 zimefungwa kote kaskazini-magharibi mwa Nigeria, na hata pale shule zinapoendelea kufanya kazi, baadhi ya wazazi wanahofia kuwapeleka watoto wao.

Chanzo: rtre