1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Wanafunzi 35 wa Chuo Kikuu watekwa nyara Nigeria

22 Septemba 2023

Watu waliojihami kwa silaha nchini Nigeria wamewateka watu 35 kutoka chuo kikuu cha kaskazini-mashariki mwa Zamfara leo Ijumaa, katika tukio kubwa la utekaji linalowahusisha wanafunzi mwaka huu.

 Nigeria
Msichana katika jimbo la Zamfara NigeriaPicha: Afolabi Sotunde/REUTERS

Watu waliojihami kwa silaha nchini Nigeria wamewateka watu 35 kutoka chuo kikuu cha kaskazini-mashariki mwa Zamfara siku ya Ijumaa, katika tukio kubwa la utekaji linalowahusisha wanafunzi mwaka huu.

Magenge ya silaha yameshamiri katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, yakiteka watu kwa ajili ya kikomboleo, kupora na kuharibu jamii na kuwaua raia.

Majaribio ya vikosi vya usalama kusitisha ghasia za makundi hayo yamekuwa na ufanisi mdogo. 

Baadhi ya wasichana wa Chibok waliookolewa baada ya kutekwa 2017Picha: Sunday Aghaeze/AFP

Msemaji wa gavana wa Zamfara, Mugira Yusuf, amesema wanafunzi 24, wafanyakazi 10 na mlinzi walitekwa na watu wenye silaha mapema Ijumaa, kutoka chuo kikuu cha shirikisho cha Gusau.Wabeba silaha waua 3, wawateka 20 chuoni Nigeria

Utekaji wa wanafunzi, ambao zamani ulikuwa unatumiwa na makundi ya wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu kuwatishia raia, umegeuka kuwa sekta ya kuchuma pesa na magenge ya uhalifu yanayoomba fidia.