1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Wanafunzi wafariki baada ya shule kuporomoka Nigeria

12 Julai 2024

Shule moja imeporomoka katika eneo la kati mwa Nigeria na kusababisha vifo vya wanafunzi kadhaa, hadi sasa miili saba ya wanafunzi tayari imetolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo hilo la shule.

Waokoaji wakiendelea na shughuli ya uokoaji Nigeria
Waokoaji wakiendelea na shughuli ya uokoaji NigeriaPicha: NEMA Nigeria/X

Baadhi ya wanafunzi walionasa kwenye vifusi wamesikika wakilia na kuitisha msaada. Shirika la kitaifa la kushughulikia majanga nchini humo NEMA, katika taarifa limesema, jengo la gorofa mbili lililokuwa shule ya Saint Academy katika mji wa Busa Buji huko Jos, ndilo lililoporomoka.

Maafisa hawajatoa idadi kamili ya wanafunzi waliofariki ingawa mkaazi mmoja wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa anakadiria watu 8 wamefariki katika eneo hilo la tukiona dazeni kadhaa kujeruhiwa.

Chanzo cha tukio hilo hakijabainika ila wakaazi wanasema tukio hilo limejiri baada ya siku tatu za mvua kubwa katika eneo hilo tambarare.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW