Wanafunzi wataka vyuo vikuu vifungwe
7 Oktoba 2016Maandamano ya wanafunzi wanaopigania usawa kwenye fursa ya kupata elimu yamevilazimisha baadhi ya vyuo vikuu, vikiwemo Witswatersrand na Cape Town, kuahirisha masomo mara mbili katika kipindi cha mwezi mmoja.
Chuo Kikuu cha Wits kilitarajiwa kuanza tena masomo hapo Jumatatu (3 Oktoba), lakini kukatokea mapambano kati ya wanafunzi na polisi katika kampasi ya chuo hicho.
Katika taarifa yake, chuo hicho kilisema kwamba hakikufikia makubaliano na wanafunzi waliokuwa wakiandamana juu ya kuanza tena kwa masomo siku ya Jumatatu inayofuata (Oktoba 10).
Gharama za elimu ya juu inayopingwa na wanafunzi wengi weusi imekuwa kiashiria cha kutokuwepo kwa usawa unaoendelea kuikumba Afrika Kusini kwa zaidi ya miongo miwili baada ya kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo.