1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa yapiga marufuku Abaya shuleni

2 Septemba 2023

Wanafunzi watakaovalia mavazi aina ya abaya au baibui hawataruhusiwa kuingia madarasani nchini Ufaransa. Haya yamesemwa na rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron jana Ijumaa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akihudhuria mkutano wa dharura wa serikali wakati wa maandamano nchini humo mnamo Juni 30, 2023
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Yves Herman/AP/picture alliance

Rais Macro ameeleza kwamba mamlaka zitakuwa thabiti katika kutekeleza sheria hiyo mpya, masomo yatakapoanza tena wiki ijayo.

Wakati wa mkutano na wanahabari siku nne zilizopita, waziri wa elimu nchini humo Gabriel Attal alitangaza kuwa nguo zinazovaliwa hasa na waislamu zinazojulikana kama abaya kwa wasichana na wanawake na khamis kwa wavulana na wanaume, zitapigwa marufuku wakati wa kuanza kwa mwaka mpya wa shule siku ya Jumatatu.

Wanafunzi watakaovaa mavazi marefu watakiuka kanuni ya msingi ya Ufaransa

Macron alizungumzia kanuni hiyo ya mavazi kwa mara ya kwanza hadharani baada ya kutembelea shule moja katika eneo la Vaucluse kusini mwa Ufaransa.

Macron amesema anajuwa kutakuwa na visa vya wanafunzi kuijaribu sheria hiyo pamoja na wale watakaojaribu kupinga mfumo huo.
 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW