1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHong Kong

Wanaharakati 45 wahukumiwa vifungo jela huko Hong-Kong

19 Novemba 2024

Makumi ya wanaharakati mashuhuri huko Hong-Kong wamehukumiwa hivi leo hadi miaka 10 jela.

Hong- Kong | Usalama ukiwa umeimarishwa nje ya jengo la Mahakama
Usalama ukiwa umeimarishwa nje ya jengo la Mahakama huko Hong-KongPicha: Tyrone Siu/REUTERS

Hatua hii imechukuliwa katika kesi kubwa zaidi inayowahusisha na vitendo vya kuhatarisha usalama wa taifa.

Washtakiwa hao wapatao 47 na waliofunguliwa mashitaka mwaka 2021, walikuwa wakikabiliwa na kifungo cha maisha jela chini ya sheria kali iliyowekwa na Beijing na iliyokandamiza vuguvugu la kuunga mkono demokrasia ambalo lilijizolea umaarufu mkubwa.

Washtakiwa 45 aidha walikiri  shitaka la kula njama ya kufanya uasi  au walipatikana na hatia na majaji watatu walioidhinishwa na serikali kuhusu mipango ya wanaharakati hao ya kuleta mabadiliko kupitia uchaguzi usio rasmi ambao ungeidhoofisha mamlaka ya serikali katika mji huo wa Hong-Kong na kusababisha mgogoro wa kikatiba.

Hata hivyo washtakiwa wawili kati ya hao wameachiwa huru. Waangalizi wanasema kesi hiyo inaonyesha ni kiasi gani mamlaka inavyokandamiza upinzani na vyombo vya habari kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali ya mwaka 2019.