1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati Tanzania walaani kukamatwa wanaopinga DP World

Florence Majani15 Agosti 2023

Wadau wa haki za binadamu Tanzania na mashirika ya kimataifa wamelaani kitendo cha kukamatwa kwa wanasiasa na wanaharakati wanaopinga mkataba wa bandari na kampuni ya DP World ya Dubai

Tansania | Hafen in Dar es Salaam
Picha: Xinhua/picture alliance

Wadau wa haki za binadamu Tanzania na mashirika ya kimataifa wamelaani kitendo cha kukamatwa kwa wanasiasa na wanaharakati wanaopinga mkataba wa bandari  na kampuni ya DP World ya Dubai akiwamo mwanasiasa mkogwe Tanzania, Dk Wilbroad Slaa, na kuzitaka mamlaka kuwaachia watu hao bila masharti yoyote. 

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya polisi kumshikilia Mwanadiplomasia huyo, jumapili ya Agosti 13, akiwa katika mjadala wa kisiasa uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia mtandao wa kijamii wa Club House.

Akizungumza na DW Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Ana Henga amesema, wanalaani kitendo cha serikali kuwakamata wanaopinga mkataba kati ya serikali na kampuni ya DP World ya Dubai.

Mwanasiasa mkongwe Slaa ni miongoni mwa walioshikiliwaPicha: DW/M.Khelef

Soma pia: Mahakama Kuu Tanzania yabariki mkataba wa bandari

Pamoja na LHRC Wadau wenginbe ambao wameungana kutoa tamko la kulaani kamata kamata hiyo ni Watetezi wa haki za binadamu(THRDC), Jukwaa la Katiba (JUKATA) na Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS).

Pamoja na watetezi wa kutoka nchini, pia Shirika la utetezi wa haki za binadamu la kimataifa, Amnesty International limetoa taarifa leo na kuzitaka mamlaka za nchini hapa kuwaachia mara moja, bila masharti, Slaa, na wakili Boniface Mwabukusi, na mwanaharakati Mdude Nyagali.

Wakati huo huo, utata umegubika juu  ya wapi alipo  Dk Slaa baada ya kutopatikana katika vituo vya polisi alimowekwa tangu alipokamatwa jumapili Agosti 13.

Msemaji wa familia, na wakili wa Dk  wa mwanasiasa huyo ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Chadema Taifa, Dickson Matata amesema.

Hata hivyo Matata amesema, huenda mwanasiasa huyo amesafirishwa kwenda Mbeya ili kujumuishwa na wenzake, ambao walikamata tangu Agosti 12 mwaka huu.

Kamata kamata hii ilianzia kwa Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanaharakati wa kisiasa, Mdude Nyagali ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kukosoa mkataba wa bandari ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai.

Hivi karibuni Mkuu wa Majeshi nchini IGP Camilius Wambura aliwaonya wale aliowataja kuwa wanapanga njama ya kumpindua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW