Wanaharakati Tanzania wataka mabadiliko ya uchaguzi
9 Machi 2018
Kesi ya kikatiba inayopinga wakurugenzi wa manispaa na wateule wa rais kusimamia uchaguzi, ambayo imefunguliwa na kundi la wanaharakati na kuongozwa na wakili Fatma Karume, imetajwa leo katika Mahakama Kuu Tanzania.
Kesi hiyo ilifunguliwa rasmi tarehe 27 Februari. DW imezungumza na wakili Fatma Karume na kwanza kuuliza kipi kilichowafikisha asubuhi ya leo katika ofisi ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam