1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wapongeza kuwabatiza waliobadili jinsia

11 Novemba 2023

Wanaharakati wa haki za mashoga wamepongeza tamko la Vatican, lililotoa ruhusa ya kubatizwa kwa watu waliobadili jinsia chini ya misingi sawa na ile inayotoa ubatizo kwa waumini wengine.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa FrancisPicha: Marco Bertorello/AFP

Miongoni mwa waliosifu hatua hiyo ni kasisi wa tawi la kijesuti ambalo ni sehemu ya kanisa katoliki  James Martin pamoja mchungaji Jean-Michel Dunand ambaye ni mwanzilishi wa kanisa linalotoa huduma kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Soma zaidi: Papa ashutumu ushoga kufanywa uhalifu

Wawili hao wamesema muongozo wa Vatican wa kuruhusu kubatizwa kwa watu waliobadili jinsia, wale wanaolelewa na wapenzi wa jinsia moja au watoto waliozaliwa na mwanamke aliyebeba mimba kwa niba ya mtu mwingine ni hatua moja mbele kuelekea ujumuishi ndani ya kanisa katoliki.

Kwenye waraka uliochapishwa siku ya Jumatano na kuidhinishwa na Papa Francis, kanisa limeridhia kubatizwa kwa watu hao lakini kwa tahadhari kwamba zoezi hilo halitazusha kashfa au mivutano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW