Sheria na Haki
Wanaharakati wakosoa kukamatwa kwa Bobi Wine
21 Agosti 2018Matangazo
Kwa mujibu wa ripoti, wabunge hao wako katika hali inayotia hofu baada ya kupigwa. Waandamanaji ambao wamekuwa wakijitokeza pia wamekabiliwa na nguvu za vyombo vya dola na mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi. Je, watetezi wa haki za binaadamu katika mataifa jirani wanayaangalia vipi matukio hayo ?John Juma amezungumza na mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za binadamu "Article 19" Afrika Mashariki, Henry Maina akiwa Nairobi Kenya, na kwanza anaelezea juu ya mtizamo wake kuhusu kile kinachotokea nchini Uganda.