1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

kamanda wa IS adaiwa kujiripua Uturuki ilipojaribu kumkamata

1 Mei 2023

Shirika moja la kutetea haki za binadamu limesema kuwa kamanda mmoja wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS alijiripua wakati majeshi ya Uturuki yalipokuwa yanajaribu kumkamata kaskazini mwa Syria.

Rami Abdel Rahman
Picha: Getty Images/AFP/L. Neal

Rami Abdel Rahman ambaye ni mkuu wa shirika la Syrian Observatory for Human Rights ametoa taarifa hiyo kwa shirika la habari la Ujerumani dpa ingawa hakuweza kuthibitisha iwapo ndiye mkuu wa kundi hilo.

Shirika hilo linasema tukio hilo limetokea Janderes katika eneo la Afrin.

Erdogan: Vikosi vya Uturuki vimemuua Kiongozi wa IS

Hapo jana Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliliambia shirika la habari la Uturuki TRT Turk, kwamba mtu huyo ni Abu Hussein al-Qurayshi na ambaye aliuwawa na majeshi ya Uturuki katika operesheni iliyofanywa Jumamosi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW