1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wataka walemavu walindwe dhidi ya joto kali

26 Juni 2023

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limezitaka mamlaka za nchi za Ulaya, kutowa usadizi wa kutosha kwa walemavu, katika msimu huu wa joto kali

Symbolbild: Extremes Wetter
Picha: Jorge Guerrero/AFP/Getty Images

Shirika hilo limesema watu wenye ulemavu nchini Uhispania na katika nchi nyingine za Ulaya wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa sana kutokana na hali ya joto na jua kali katika kipindi cha kiangazi.

Katika ripoti yake, shirika hilo limesema walemavu wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha, kuumizwa kimwili, kisaikolojia na matatizo ya afya ya kiakili kutokana na joto kali na hasa wanapoachwa kujishughulikia wenyewe wakati kukiwa na hali hatari ya viwango vikubwa vya joto.

Jonas Bull, mtafiti msaidizi  katika shirika la Human Rights Watch amesema hali ya kushindwa kufikika maeneo mbali mbali katika maeneo ya mijini imechangia kuongeza matatizo kwa walemavu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW