1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati: Watu 6,126 waliuawa Iran

27 Januari 2026

Wanaharakati wanasema kiasi watu 6,126 waliuawa kufuatia hatua kali dhidi ya waandamanaji nchini Iran, huku kukiwa na wasiwasi ya vifo zaidi.

Takwimu hizi za leo zimetolewa na Shirika la Wanaharakati wa Haki za Binaadamu lenye makao yake nchini Marekani lililothibitisha kila kifo kwa kushirikiana na mtandao wa wanaharakati wa ndani ya Iran.

Kulingana na takwimu hizo, waandamanaji 5,777 waliuawa wanajeshi 214 wenye mafungamano na serikali, watoto 86 na raia 49 ambao hawakuandamana. Watu 41,800 walikamatwa.

Serikali ya Iran ilisema idadi ya waliouawa haikuzidi 3,117 na kusema 2,427 walikuwa ni raia na wanajeshi wa vikosi vya usalama, huku ikiwataja wengine kama magaidi.

Hayo yanaelezwa, huku taarifa zikisema manowari ya kijeshi ya Marekani tayari imewasili eneo la Mashariki ya Kati kuongoza hatua zozote za kijeshi za Marekani za kushughulikia mzozo huo.

 

Tanbihi ya Mhariri: Makala hii awali ilijumuisha picha kutoka shirika la SalamPix. Iliondolewa tarehe 12 Machi 2026 baada ya Picture Alliance na Imago kutuarifu kuwa walikuwa wanaondoa picha za SalamPix kutokana na wasiwasi kuhusu chanzo chake na uwezekano wa kuwa zimehaririwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW