1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Wanajeshi 10 wauawa kwenye mapigano Yemen

22 Machi 2023

Wanajeshi wasiopungua 10 wameuawa kwenye mapigano ambayo yamezuka upya nchini Yemen. Duru za kiusalama zimeliambia shirika la habari la AFP.

Soldaten im Jemen nehmen an einer Militärparade zur Feier der Vereinigung des Jemen teil
Picha: AP

Hayo yamejiri licha ya juhudi za kidiplomasia za kusitisha vita hivyo ambavyo vimedumu kwa muda mrefu kwenye taifa hilo maskini zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu.

Mapambano yalitokea katika mkoa unaozalisha mafuta wa Marib ambao pia ni mojawapo ya maeneo makuu ya mapigano ya mara kwa mara tangu mwaka uliopita.

Vyanzo viwili vya habari vya kijeshi vimeiambia AFP kwamba waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran na ambao wamekuwa wakiongeza idadi ya wapiganaji wao, waliyashambulia maeneo ya mlima mkoani humo.

Wanajeshi 10 wamethibitishwa kufariki kwenye mashambulizi hayo pamoja na idadi isiyojulikana ya washambuliaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW