Wanajeshi 20 wa uturuki wafariki dunia katika ajali ya ndege
12 Novemba 2025
Matangazo
Wizara ya ulinzi ya Uturuki mapema Jumatano imechapisha picha za wanajeshi hao 20 waliofariki dunia katika mtandao wa kijamii wa X.
Shirika la habari la Uturuki Anadolu limeripoti kuwa sababu ya ajali hiyo ya ndege bado haijajulikana.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Azerbaijan kuelekea Uturuki na kulingana na wiazara ya mambo ya ndani ya Uturuki, ilianguka karibu kilomita tano tu kutoka mpaka wa Azerbaijan.
Mamlaka zinachunguza iwapo ukiukaji wa sheria za usafiri wa angani ulichangia ajali hiyo.