1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

wanajeshi 200 zaidi wa Ufaransa wawasili Libnan

9 Septemba 2006

Meli iliyosheheni wanajeshi 200 wa Ufaransa imetia nanga katika bandari ya mjini Beyrouth nchini Libnan.Wanajeshi hao watapelekwa kusini mwa Libnan kusaidiana na vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani UNIFIL..Wanajeshi zaidi wa Ufaransa wanasubiriwa kuwasili Libnan wiki zijazo.Wengine 250 wameshawasili katika eneo hilo.Kabla ya hapo manuari za kijeshi za nchi za ulaya zilianza kupiga doria kulinda fukwe za Libnan chini ya usimamizi wa Italy.Manuari hizo zinajukumu la kuzuwia biashara haramu ya silaha wanazopatiwa wanamgambo wa Hisbollah.Duru za Ufaransa zinasema wanamaji hao hawajapewa jukumu la kutumia nguvu kuzuwia meli zinazopita baharini.Imepangwa kuikabidhi Ujerumani uongozi wa ulinzi wa fukwe za Libnan.