1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

Wanajeshi 3 wa Marekani wafariki katika ajali ya ndege

27 Agosti 2023

Ndege ya kijeshi ya Marekani imeanguka kaskazini mwa Australia hii leo na kusababisha vifo vya wanajeshi wake watatu na wengine 20 kujeruhiwa wakati wakifanya mazoezi ya kijeshi.

Wafanyakazi wa huduma za afya wakiwa na kitanda cha kwapokea wanajeshi waliokimbizwa hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye anjali ya ndege
Wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa walipekwa kwenye hospitali iliyoko mji wa Darwin kufanyiwa matibabuPicha: /AUSTRALIAN BROADCASTING CORPORATIONREUTERS

Wanajeshi hao watatu wa Marekani wamethibitishwa kufa katika ajali hiyo iliyotokea katika kisiwa cha Melville huku wengine watano kati ya 23 waliokuwa ndani ya ndege waliojeruhiwa vibaya na wakikimbizwa katika hospitali ya mji wa Darwin.

Taarifa zimesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema ni wamarekani tu ndio walioumia katika mazoezi hayo yaliyohusisha wanajeshi wa Marekani, Australia, Indonesia, Ufilipino na Timor ya Mashariki.

Amesema serikali kwa sasa itajikita katika kukichunguza kisa hicho na kutoa msaada wa kila hali katika wakati huu mgumu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW