1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Wanajeshi 47 wauawa katika shambulio la kigaidi Niger

27 Juni 2024

Makundi ya kigaidi nchini Niger yamefanya mashambulizi mabaya zaidi dhidi ya wanajeshi kuwahi kushuhudiwa kwa muda mrefu.

Miili 47 ya wanajeshi wa Niger ilipatikana baada ya mashambulizi katika eneo la mpaka la Mali na Burkina Faso.
Miili 47 ya wanajeshi wa Niger ilipatikana baada ya mashambulizi katika eneo la mpaka la Mali na Burkina Faso.Picha: Gazali/DW

Ripoti zimesema wapiganaji wenye silaha nzito waliokuwa kwenye pikipiki na magari ya kivita waliishambulia kambi iliyo karibu na Gothèye, iliyopo kama kilomita 80 kutoka mji mkuu Niamey.

Miili 47 ya wanajeshi wa Niger ilipatikana baada ya mashambulizi katika eneo la mpaka la Mali na Burkina Faso kuendelea Jumanne asubuhi, hii ikiwa ni kulingana na vyanzo vya kijeshi na vya eneo hilo walipozungumza na shirika la habari la dpa huko Niamey jana Jumatano.

Aidha, watu 18 waliripotiwa kujeruhiwa, 11 vibaya na wanajeshi kadhaa pia hawajulikani walipo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW