1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurkina Faso

Wanajeshi 50 wa Burkina Faso wauwawa kwenye shambulizi

21 Februari 2023

Wanajeshi wasiopungua 51 wa Burkina Faso wameuwawa katika shambulizi la kustukiza lililotokea eneo la kaskazini mwa nchi hiyo linalofahamika kwa hujuma kubwa za makundi ya itikadi kali.

Burkina Faso | Soldaten in Kaya
Picha: Sophie Garcia/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyotolewa jana na jeshi la Burkina Faso  imesema wanajeshi hao walishambuliwa kwenye jimbo la Oudalan ambalo linaitenganisha nchi hiyo na taifa jirani la Mali.

Shambulizi hilo ambalo linatajwa kuwa limesababisha idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi kwa wakati mmoja tangu kuzuka kwa uasi wa makundi ya itikadi kali nchini humo limetokea siku mbili kabla ya Ufaransa kuhitimisha operesheni zake za kijeshi nchini humo.

Katika mkasa mwingine uliotokea kwenye jimbo lingine la kaskazini mwa nchi hiyo, wanamgambo wenye silaha  wamewateka nyara wanawake 50 waliokuwa msituni kutafuta chakula. Serikali imesema imeanzisha msako wa kuwatafuta na kuwaokoa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW