Wanajeshi 70 wa Ukraine wauwawa
1 Machi 2022Kwa sasa pia serikali inasema msururu wa msafara wa wanajeshi wa Urusi unakaribia katika maeneo ya mji wa Kyiv. Hadi wakiti huu kuwepo kwa makabiliano makali kumekanushwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin ambae ameeleza kupatikana ushindi katika hatua za mapema kufuatia mapigano hayo ambayo yanatajwa kujwa makubwa tangu kumalizika Vitu Vikuu Vya Pili vya Dunia.
Msafara wa majeshi ya Urusi wa kilometa 64 kuelekea Kyiv
Mtandao wa satelaiti wa kampuni ya Kimarekani ya Maxaer unasema Urusi imekusanya msururu wa magari ya kivita, vifaru na vifaa vingine vya kijeshi katika urefu wa kilometa 64 ukionena kuelekea Kyiv.
Katika nyongeza ya hilo wizara ya Ulinzi ya imesema taarifa zake za kijasusi Urusi imeongeza matumizi ya makombora ya mizinga mikubwa. Imesema hatua hiyo katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu inahatarisha athari zaidi.
Madai ya mashambizi katika maeno ya kijeshi ya Ukraine
Vikosi vya Urusi vimekuwa vikishambulia maeneo mbalimbali ya kujikinga ya Ukraine, na maafisa wa Ukraine wameripoti pia matukio ya mashambulizi ya mambomu katika mji wa Kharkiv, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo ambapo watu kadhaa wanaripotiwa kuuwawa.
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Oleksii Reznikov amesikika akisema mashambuli mengi ya reketi kutoka kwa mahasimu wao dhidi ya miji iliyotulivu yanatoa ushahidi tosha kuwa wameshindwa kukabiliana na jeshi la Ukraine. Katika ukurasa wake wa Facebook waziri huyo ameandika wanajeshi 70 wameuwawa katika mashambulizi ya jana Jumatatu katika mji wa kati ya Kharkiv na Kyev.
Kuuwawa kwa wanajeshi zaidi ya 5,710 wa Urusi
Mkuu wa majeshi wa Ukraine anasema imepoteza wapiganaji 5,710 kushambulia ndger 29 na vifaru 198, idadi ambayo hata hivyo imekuwa ngumu kuthibitishwea.
Kwa upande mwingine mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine yanaelezwa kushindwa kutoa matokeo yoyote na wajumbe pia hawajasema lini duru ya pili ya mazungumzo hayo itarejea mezani.
Hali ya ukimbizi inaendelea kuwa mbaya takribani watu 350,000 wameingia Poland hadi sasa. Waziri wa Mambo ya Ndani ya taifa hilo anasema katika kipindi cha masa 24 watu 100,000 wameingia kutoka Ukraine.
Chanzo: AP