Wanajeshi wa Guatemala na El Salvador wawasili Haiti
4 Januari 2025Zaidi ya wanajeshi 80 kutoka Guatemala na El Salvador waliwasili Haiti siku ya Ijumaa kama sehemu ya ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na Kenya ili kuimarisha jeshi la polisi kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya kihalifu.
Hadi Kufikia sasa, kuna maafisa 400 wengi wao wakiwa Wakenya, lakini pia baadhi kutoka Jamaica na Belize kati ya 2,500 wanaotarajiwa.
Lakini kikosi hicho hakina vifaa vya kutosha huku kikijaribu kukomesha magenge yenye nguvu na yenye silaha nchini Haiti. Magenge hayo yameshutumiwa kwa mauaji, ubakaji na utekaji nyaraili kujipatia fidia.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa magenge hayo yanadhibiti takriban asilimia 85 ya mji mkuu wa Port-au-Prince. Vurugu za magenge hazijakoma katika nchi hiyo iliyokumbwa na mzozo ya Caribbean tangu jeshi la kimataifa lilipowasili.