1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Bundeswehr hawatotupa mabomu

4 Desemba 2015

Wabunge wa Ujerumani wameunga mkono mpango wa kutumwa wanajeshi hadi 1200 na ndege za upelelezi kushiriki katika opereshini za kimataifa dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam IS nchini Syria.

Kanasela Angela Merkel akipiga kura bungeni kuamua juu ya kutumwa wanajeshi wa Ujerumani kupambana na IS nvchini SyriaPicha: Reuters/H. Hanschke

Kama ilivyokuwa ikitarajiwa bunge la shirikisho,Bundetag limeidhinisha kwa wingi mkubwa, sauti 445 dhidi ya 146 na saba za wabunge waliojizuwia kuelemea upande wowote,mpango wa serikali ya kansela Angela Merkel inaodhibiti wingi mkubwa wa viti kutoka vyama ndugu vya Christian Democratic na Christian Social Union-CDU/CSU na wasocial Democratic wa SPD. Wabunge wa

Vyama vya upinzani vya walinzi wa mazingira die Grüne na die Linke wanaupinga mpango huo wakihoji hautosaidia kuwapunguzia dhiki na usumbufu wananchi wa Syria. Mwenyekiti wa chama cha siala kali za mrengo wa kushoto die Linke,bibi Sahra Wagenknecht anasema;"ita vinaifanya hali izidi kuwa mbaya.Hawatowaandama wanamgambo wa IS,wakipelekwa huko watazidi kuwapa nguvu."

Mpango huo unataja juu ya kutumwa wanajeshi hadi 1200 mwaka 2016-hiyo ikiwa idadi kubwa kabisa ya wanajeshi wa Ujerumani Bundeswehr kuwahi kutumwa nchi za nje.Serikali ya Berlin inapanga pia kutuma ndege sita chapa Tornado nchini Uturuki ili kushiriki katika shughuli za upelelezi nchini Syria pamoja na manuari itakayosaidiana na ile ya Ufaransa inayobeba ndege za kivita-"Charles de Gaule".

Wanajeshi wa Ujerumani hawatoshiriki katika mapigani ya nchi kavu

Tarehe ya kushiriki katika opereshini hizo bado haijatangazwa.

Ndege ya upelelezi ya Ujerumani,TornadoPicha: Reuters/F. Bimmer

Jeshi la Ujerumani halitoshiriki katika opereshini zozote za kutupa mabomu,kinyume na wanavyofanya wanajeshi wa Ufaransa au wa Marekani na tangu alkhamisi pia Uengereza iliyoanza kuvurumishja mabomu mara baada ya kupata idhini ya bunge la nchi hiyo.

Waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Ursula von der Leyen ameupongeza uamuzi wa bunge huku akishadidia jukumu wanalotwikwa wanajeshi ni "la hatari".Waziri von der Leyen ameondowa hata hivyo uwezekano wa kushiriki wanajeshi wa Ujerumani siku za mbele katika vikosi vya nchi kavu nchini Syria.

Kwa upande wake katibu wa dola wa Ufaransa anaeshughulikia masuala ya Umoja wa ulaya,Harlem Désir amesifu uamuzi wa bunge la Ujerumani akisema ni "ushahidi wa mshikamano wa kipekee wa Ujerumani kwa Ufaransa."

Rais Hollande azuru manuari Charles de Gaule

Uamuzi wa bunge ni jibu kwa maombi ya Ufaransa baada ya mashambuilio ya kigaidi ya Novemba 13 yaliyoangamiza maisha ya watu 130 mjini Paris.

Ndege ya kivita ya Ufaransa Rafale inayofyetuliwa toka manuari ya Charles de GaulePicha: picture alliance/dpa/Ecpad Handout

Wakati huo huo rais wa Ufaransa Francois Hollande anaizuru manuari inayobeba ndege za kivita Charles de Gaule iliyotia nanga karibu na fukwe za Syria.Kupelekwa manuari hiyo ya Ufaransa katika fukwe za mashariki za bahari ya Mediterenia kunazidisha mara tatu nguvu za ndege za kivita za Ufaransa katika opereshini zake nchin i Syria na Iraq.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/dpa/Reuters

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW