1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Wanajeshi sita wa Ukraine wauwa katika ajali ya ndege

31 Agosti 2023

Wanajeshi sita wa Ukraine wamepoteza maisha baada ya ndege mbili za kijeshi aina ya Helikopta kuanguka zikiwa zinakwenda katika opresheni ya kijeshi Mashariki mwa nchi hiyo.

Die Wagner-Gruppe - Russlands Söldner in Libyen
Picha: Journeyman

Idara ya uchunguzi ya  serikali SBI imetoa taarifa hiyo leo ikisema helikopta  hizo mbili za kijeshi chapa Mi-8  zilianguka Jumanne katika wilaya ya Kramatorsk,katika jimbo la Mashariki la Donetsk ingawa hakuna ufafanuzi wa kina uliotolewa kuhusu kilichotokea. 

Soma pia:Urusi yasema imedungua droni ya Ukraine iliyoelekezwa Moscow

Taarifa hiyo pia imeleeza kwamba uchunguzi wa awali unaofanywa na shirika la ujasusi kuhusu masuala ya usalama nchini humo utajikita kuangalia ikiwa kuna uwezekano sheria za kiusalama zilikiukwa wakati na baada ya ndege hizo kuanza safari.

Jambo ambalo linaweza kushughulikiwa kama kosa la uhalifu. Nyingi ya helikopta hizo chapa Mi-8 za Ukraine ni za miongo kadhaa.  
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW