Wanajeshi wa Burkina Faso Na Mali wakutana kujadili usalama
3 Novemba 2022Kiongozi mpya wa kijeshi nchini Burkina Faso kapteni Ibrahim Traore amefanya ziara mjini Ouagadougou Mali, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipochukua madaraka kupitia mapinduzi mnamo Septemba 30 mwaka huu.
Kiongozi mwenzake wa Jeshi nchini Mali kanali Assimi Goita amesema ziara hiyo ni muhimu kwa ajili ya amani na usalama wa mataifa hayo mawili.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter Kanali Goita aliyeingia madarakani pia kupitia mapinduzi Agosti mwaka 2020 amesema wamezungumza kwa upana kuhusu changamoto za kiusalama zinazozikumba nchi hizo.
Awali afisa mmoja wa Burkina faso alisema viongozi hao wawili watajadili vita dhidi ya ugaidi akimaanisha changamoto ya mataifa hayo kupambana na makundi ya wanamgambo walio na itikadi kali. Mataifa hayo ya Sahel yameorodheshwa kuwa miongoni mwa mataifa masikini na yasiyo na utulivu duniani.