1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Wanajeshi wauwawa Chad katika mapambano na Boko Haram

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Wanajeshi kadhaa wameuwawa nchini Chad baada ya makabiliano na wanamgambo wenye Itikadi kali wa Boko Haram katika mkoa wa Ziwa Chad.

Chad
Kiongozi wa Chad Mahamat Idriss DebyPicha: Gilles Chris Namia Rimbarne/REUTERS

Vyanzo vya kijeshi vinasema mapigano yalitokea mchana kwenye kisiwa cha Karia Kaskazini Magharibi mwa mkoa huo. "Afisa kutoka ofisi ya mkuu wa utumishi wa jeshi aliyeomba  kutotajwa jina amesema maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wameuwawa katika shambulio hilo.

Soma zaidi: Chad yadai imewauwa wanamgambo wengi wa Boko Haram

Kufuatia ripoti hizo Rais Mahamat Idriss Deby Itno ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wanajeshi waliouwawa, na kuwatakia ahueni majeruhi kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Mapambano hayo ndiyo ya karibuni zaidi tangu yale ya mwishoni mwa mwezi Oktoba yaliyofanywa na Boko Haram na kuilenga kambi ya jeshi. Shambulio hilo liliwauwa takriban watu 40. Jeshi la Chad katika kulipa kisasi lilianzisha operesheni dhidi ya wanamgambo hao wenye itikadi kali za Kiislamu.