1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Wanajeshi wa Eritrea waondoka kaskazini wa Ethiopia

30 Desemba 2022

Wanajeshi wa Eritrea wameanza kuondoka kwenye miji ya Shire na Axum katika jimbo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.

Äthiopien I Konfliktregion Tigray
Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Haikufahamika mara moja iwapo vikosi vya Eritrea vilikuwa vinaondoka kabisa Tigray au vilikuwa vinaondoka tu kwenye miji kadhaa.

Waziri wa Habari wa Eritrea, Yamane Gebremeskel ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hawezi kuthibitisha au kukanusha kama wanajeshi wanaondoka.

Vikosi vya Eritrea bado vyatekeleza mauaji ya raia wa Tigray

Wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada huko Axum na Shire wamesema wameona malori na magari kadhaa yaliyojaa wanajeshi wa Eritrea wakiondoka jana kuelekea kwenye mpaka wa Sheraro.

Eritrea yadaiwa kufanya mashambulizi katika mpaka wake na Ethiopia

Wakati huo huo, polisi wa Ethiopia wameanza kupelekwa kwenye jimbo la Tigray kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 18, baada ya makubaliano ya amani kufikiwa, takribani miezi miwili iliyopita.

Polisi imesema kulingana na mamlaka waliyopewa na katiba ya kulinda taasisi za shirikisho, jana waliingia Mekele na wameanza kazi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW