Wanajeshi wa India wajitahadharisha
14 Agosti 2005Matangazo
New Delhi:
Wanajeshi wa India leo wameweka mizinga ya kutungua ndege, walenga shabaha, wamefunga majengo na kuweka vizuizi vya barabarani mjini New Delhi siku moja kabla ya kusherehekea uhuru wa nchi hiyo. Wahindi kesho Jumatatu watasherehekea miaka 58 ya uhuru wao kutoka kwa Waingereza mwaka 1947. Kutakuwa na magwaride, sherehe za kupandisha bendera na matafrija mbalimbali ya kiutamaduni. Lakini sherehe hizo mara kwa mara zimekuwa zikiambatana na mashambulio ya vikundi mbalimbali vinavyopigania uhuru wao au vinavyodai utawala wa ndani katika maeneo yanayogombaniwa ya Kashmir na kaskazini mashariki mwa India. Waasi wa Mao wanaendesha harakati zao katika sehemu nyingi za India.