1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wanajeshi wa Israel wahimizwa kuwa waangalifu

16 Desemba 2023

Wanajeshi wa Israel wametakiwa kuwa "waangalifu zaidi" kufuatia mauaji ya kimakosa ya mateka watatu wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza

Msemaji wa jeshi la Israel, Jonathan Conricus akizungumza na DW akiwa Tel Aviv
Msemaji wa jeshi la Israel, Jonathan ConricusPicha: DW

Msemaji wa jeshi hilo la IDF Jonathan Conricus amesema jeshi la Israel bado linachunguza jinsi ajali hiyo ilivyotokea lakini limebainisha kuwa wapiganaji wa Hamas wakati mwengine huvaa nguo za kiraia na kusema kwamba hali hiyo inasababisha kile alichokiita ''mazingira magumu ya mapambano." Conricus amehimiza wanajeshi wao kuwa macho hasa pale wanapoandamwa na watu waliovaa kiraia.

Conricus asema azma yao haitayumbishwa

Msemaji huyo ameongeza kuwa hata katika tukio la kusikitisha kama hilo, halitayumbisha azma yao ya kuliangamiza kundi la Hamas.

Hapo jana jioni, jeshi hilo la Israel lilikiri kuwapiga risasi mateka watatu wakati wa operesheni huko Shejaiya, eneo la mashariki mwa mji wa Gaza, na kulitaja kuwa eneo la mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea katika siku za hivi karibuni.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW