1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Israel waivamia Nablus

27 Desemba 2003
TEL AVIV: Siku mbili baada ya kufanyika shambulio la kujitolea mhanga maisha mjini Tel Aviv, wanajeshi wa Israel mkesha wa Jumamosi, wametumia vifaru kuanzisha operesheni kubwa ya kuwatafuta washutumiwa wa itikadi kali wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kijana wa Kipalestina mwenye miaka 19 aliuawa mjini Nablus wanajeshi wa Israel walipowashambulia kwa risasi vijana wa Kipalestina waliokuwa wakiwavurumishia mawe. Pia wanajeshi wa Israel walilivamia kambi la wakimbizi Balata na kutangaza marufuku ya kutoka nje. Wazara ya Mambo ya Ulinzi ya Israel ilisisitiza shabaha yake ya kutaka kuwauwa viongozi maalumu wa makundi ya itikadi kali ya Kipalestina. Nao wawakilishi wa makundi ya itikadi kali ya Kipalestina walijibu kwa kusisitiza kwamba wataendeleza mapigano yao.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW