1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Wanajeshi wa NATO waweka doria nchini Kosovo

29 Mei 2023

Walinda amani wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wameweka ulinzi katika ofisi tatu za manispaa nchini Kosovo ili kuwazuia raia wa Serbia wanaompinga meya mpya mwenye asili ya Albania.

Kosovo: Serben versuchen Sturm auf Rathäuser
Picha: Marjan Vucetic/AP/picture alliance

Polisi ilitumia gesi ya kutoa machozi katika mji wa Zvecan, kuwazuia Waserbia waliovuka vizuizi vya kiusalama na kujaribu kuingia kwenye jengo la manispaa na katika mji wa Leposavic, unaopakana na mpaka na Serbia, walinda amani wa Marekani walizungushia waya ya umeme jengo la manispaa ili kuwazuia mamia ya waandamanaji waliogadhabika.

Naibu mkuu wa chama cha Serb List amemtuhumu Waziri Mkuu wa Kosovo, Albin Kurti, kwa kuchochea wasiwasi katika eneo la kaskazini kunakokaliwa na raia wengi wa Serbia, huku Eaziri wa Mambo ya Nje, Ivica Dacic, akisema haiwezekani kwa eneo hilo kuogozwa na meya ambaye hakuchaguliwa na Waserbia wenyewe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW