1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Ufaransa hawakuhusika katika mauaji ya Rwanda

8 Septemba 2022

Majaji wa Ufaransa wametupilia mbali kesi dhidi ya wanajeshi walinda amani wa Ufaransa waliotumwa wakati wa mauaji ya halaiki ya Rwanda mnamo mwaka 1994, ambao walituhumiwa kuwa na mchango katika mauaji hayo.

Hutus begrüßen französische Soldaten
Picha: dpa/picture alliance

Walionusurika katika mauaji ya mwezi Juni mwaka 1994 katika vilima vya huko  Bisesero magharibi mwa Rwanda waliwashutumu wanajeshi wa Ufaransa kwa kuwatelekeza  kwa makusudi kwa Wahutu wenye msimamo mkali ambao waliwaua mamia ya watu katika eneo hilo ndani ya siku chache.

Baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na walionusurika na hata mashirika ya kutetea haki za binadamu, Waendesha mashtaka wa Ufaransa walianzisha uchunguzi mnamo Desemba mwaka 2005, kuhusu uwezekano wa kuhusika kwa wanajeshi hao katika uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Uamuzi uliyotarajiwa

Katika ripoti hiyo ya karibu kurasa 1,000, tume hiyo iliyoongozwa na mwanahistoria Mfaransa Vincent Duclert imetupilia mbali kesi dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa kuhusika katika mauaji ya halaiki.

Majaji waliosimamia shauri hilo, wameamua kutoendelea na kesi dhidi ya wanajeshi hao wa Ufaransa, uamuzi ambao hata hivyo ulitarajiwa na wengi.

Soma zaidi: Rwanda yailaumu Ufaransa kushindwa kuzuia mauaji ya Kimbari

Taarifa kutoka kwa Mwendesha mashtaka wa Paris Laure Beccuau, ilibaini kuwa

wachunguzi hawakuwa wamethibitisha "ushiriki wa moja kwa moja wa vikosi vya Ufaransa katika uhalifu uliofanywa katika kambi za wakimbizi, na wala haikubaini ushiriki kupitia misaada au usaidizi kwa vikosi vilivyohusika na mauaji ya halaiki.

Wachunguzi hao walitaka kesi hiyo itupwe nje tangu mwaka jana. Hata hivyo, bado kuna uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Wanahistoria waituhumu Ufaransa

Ufaransa, ambayo ilikuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya kabila la Wahutu iliyokuwa madarakani wakati huo, ilipeleka maelfu ya wanajeshi nchini Rwanda katika ujumbe wa kulinda amani ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa wakati wa mauaji ya kimbari.

Soma zaidi:Ufaransa yaifunga kesi liyozua mauaji ya kimbari Rwanda 

Mwezi Machi mwaka jana, ripoti ya kihistoria ya Ufaransa iliyokusanywa na wanahistoria ilihitimisha kuwa Paris ilikuwa na majukumu "mazito na makubwa" katika mauaji ya watu wapatao 800,000, hasa kutoka kabila la walio wachache la Watutsi.

Karibu watu 50,000 waliuawa katika eneo la Bisesero, ambalo lilionekana kuwa kimbilio na ngome ya Watutsi waliojaribu kujilinda.

Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Uhusiano kati ya Paris na Kigali waimarishwa

Wakosoaji wamekuwa wakisema kwamba Rais wa Ufaransa wakati huo Francois Mitterrand alishindwa kuzuia mauaji hayo au hata aliunga mkono serikali ya Wahutu ya Juvenal Habyarimana iliyopanga mauaji hayo.

Ziara ya Rais Emmanuel Macron mjini Kigali mwezi Mei, 2021, iliashiria kurejea kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Rwanda baada ya miongo kadhaa ya mivutano inayohusishwa na mauaji ya halaiki.

(AFP)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW