1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waondoka eneo la Kidal

24 Oktoba 2023

Wanajeshi wa Minusma wameondoka kaskazini mwa Mali kufuatia hatua ya viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waanza kuondoka nchini Mali
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waanza kuondoka nchini MaliPicha: UNJU Mission in Mali

Wanajeshi wa tume ya amani ya Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA wameondoka kambi yao ya Aguelhok katika eneo linalokabiliwa na machafuko la Kidal kufuatia amri ya watawala wa kijeshi kuwataka waondoke.

Hayo ni kwa mujibu wa duru za eneo hilo na Umoja wa Mataifa. Mwanajeshi wa MINUSMA kutoka Chad ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba wameondoka kutoka kambi yao ya Aguelhok jana Jumatatu.

Taarifa hiyo imethibitishwa na afisa mjini Bamako na maafisa wawili waliochaguliwa katika eneo hilo. Bado hakujafanyika hafla ya kuikabidhi kambi hiyo ya kaskazini mwa Mali.